CURRENCY CONVERTER
New Ads
Educationmakala mbalimbalisimulizi
SuraYa 1
Ni
miaka mitano sasa tangu nilipojikuta nikiwa katika nazingira haya yaliyogubikwa
Kwa wingiwa shida, karaha na kila aina ya uzuni. Nyumbani kwetu napakumbuka
japo nilitoka tangu kitambo baada ya maisha ya kutafuta Nile nini, nitasomaje
Na nitakuwa Na picha gani katika jamii hii ambayo humthamini binadamu kwa
kuangalia hadhi yake katika kipato yaani maisha mazuri ya kuweza kutatua maisha
yake ya wenye shida, na elimu aliyonayo mtu ndiyo alama ya kumfanya mtu
aonekane wa thamani katika jamii. Jamii iliyojaza watu wa aina mbalimbali na
wenye tabia, huruka, mwenendo na maono mbalimbali ni jamii inayofaa kwa
mwanasayansi au mtafiti yeyote kuzisoma jamii zote duniani kuwa ni nini hasa
kinazikumba familia na jamii nyingi kwa ujumla.
Kwa
aliye wakwanza kusimulia ndiye wa kwanza kuona, au pengine imemgusa kuwa wa
kwanza ama kutangulia kusema. Mbona unaongea kwa mafumbo makali ambayo yananipa
shida kuyafumbua? Aliuliza Boraman! Rafiki yangu kadili ninavyoendelea
Kunene maneno haya ambayo ama hakika yamezungukwa na kuroanishwa kwa machozi ya
uzuni mwingi kwani kwa haya ninayoyaona na ninayoyasikia yananifanya nifahamu
kuwa watu wengi katika jamii huishi kwa mashindano na kutamani wawebora kuliko
viumbe vingine hapa katika ulimwengu wa Musa. Unadai huelewi kwa fumbo hili
dogo yaani kama lingekuwa yai la mchemsho hata kibogoyo angetafuna na wewe
ungebaki kumeza mate na uso kuliokunjika kama safu za milima mikunjo. Mifano
ndiyo njia yaw ewe kunielewa.
Hapo
zamani kulikuwepo na mfalme katika kijiji cha Hira, ambacho kilitawaliwa kwa
nguvu za miungu na uchawi. Siku moja mfalme wa Hira aliitisha kikao cha dharura
ambacho hukaliwa mara moja kwa mwaka hasa katika kusherekea sherehe za mavuno
au majadiliano kuhusu majanga yaliyokikumba kijiji hicho ambayo huwa ni
mafuriko yanayosababisha mavuno hafifu, ukame unaopelekea kukauka kwa mazao, na
tetemeko la aridhi ambalo huwashitua watu hasa nyakati za usiku napengine
mchana wakati wa shughuli za kilimo au mavuno zikiendelea.
Haijawahi
kutokea mfalmekwa Hira kuwaita wanakijiji wa mambo mawili au Zaidi bali huwaita
kwa jambo mojamoja ili apate kujadili kwa kina na watu wake. Siku moja hakukuwa
na tukio lolote la kufanya watu waitwe ili kuelezwa jambo kwani ilikuwa ni
yapata mwezi wa sita, wiki ya sita, siku ya sita ya wiki, saa sita mchana na
dakika sita ndipo Mfalme aliwatuma walinzi wake wakazunguke kijijini kote
kuwapasha habari watu kuwa kesho ni siku ya saba saa saba mchana na dakika saba
ndio muda wa kila mmoja pale kijijini kuwa amefika kwa Mfalme ili kusikia
alichokiandaa kukisema.
Gafla
sauti ikasikika kutoka katika pembe nne
za nyumba ya Mfalme iliwa na ujumbe wa maneno manne yaliyosemwa baada ya dakika
nne kupita kwamba HATUTAKI UFANYE KAMA UNAVYOTAKA Mfalme alisikiliza kwa makini
lakini kutekeleza agizo alikuwa tayari ni mchelewaji. Alilia kwa maamzi yake
kuwakimbilia walinzi kuwakataza ilikuwa tayari maji yamezidi unga kwani
walikuwa wameisha kutana na vijana watano waliokuwa wameongozana na mbwa watano
na mabega yao hadi mgongoni ipo michilizi ya damu za wanyama waliowabeba
mabegani waliwambia kuwa, kesho saa saba na dakika saba ndio muda wa kuanza
kikao na Mfalme wa Hira ili aseme aliyonayo na nyie muliopata taarifa hizi basi
kumbuka kuwambia na wenzenu mtakaofanikiwa kuonana nao katika sehemu zenu za
mapumziko.
Mfalme
alipiga moyo konde na kusema sawa! Lakini siamini kuwa kusema adhima yangu ni
vibaya. Lakini mizimu yangu nipo chini ya unyayo wenu, nifanye mteule na mkuu
kuliko wote hapa kijijini kwani nimetawala miaka mingi na kwa unyenyekevu
mkubwa sana kwa nilipofikia nahitaji kuwa tofauti na watu wa kawaida. Sauti yao
ikasikika tena kwa mara nyingine ikisema kuwa japo wataka uonekane wa tofauti na wengine je? unataka miguu mitatu,
mikono mitatu au uso wa mbele na nyuma? Alitetemeka sana huku akiwa katika
majonzi ya kwanini kaamua kufanya vile bila kuuliza lakini Mfalme alijipa moyo
kwa kusema kosa siyo kosa bali kosa ni kurudia kosa. Nitaendelea ili kutimiza
hili japo nyie hampendi lakini musinihaibishe mbele ya wananchi wangu, kwani
natambua sitakiwi kuendana kinyume na ninyi wakuu wangu mliyenipa rungu hili la
kukiongoza kijiji hiki yapata miaka sabini tangu nikiongoza nikiwa na miaka
saba.
Akiwa
anajibizana na mizimu ya kuzimu, gafla waliludi walinzi na kukaa chini pia kunyoosha
miguu mbele na mikono kuilaza mapajani kisha mmoja wao wawili akasema kwa sauti
ya kusikika vizuri MTUKUFU MFALME!! Mfalme alishituka sana na kujikuta
kamukanyaga, Kahiramulinzialiyeagizwa na Mfalme kuwa waambatane kusambaza
habari hizo, Kahira hakuwa na shaka la kukatisha maneno yake japo kama ilivyo
kwa binadamu alishituka lakini baadae akaendelea japo alirudia kusema mtukufu mfalme kazi uliyonituma nimeifanya
kadili ya unavyotaka na kufika kesho saa saba kamaili katika sekunde ya saba watu watakuwa wamejaa hapa
kama kwenye soko la mitumba hasa karibia sherehe za krismas. Mfalme alijibu
kuwa kama umefanya kama nilivyokutuma asante sana japo ni jukumu lako. Pia Kahira alisema pia mtukufu mfalme, kwa
bahati mbaya zaidi nimejikuta nimeweka mguu wangu chini ya mguu wako huo wa
kushoto. hivyo, nisamehe sana mtukufu mfalme kama itakupendeza naomba nitoe
mguu wangu. Mfalme alicheka sana na kuendelea kuamini kuwa yeye ni kila kitu na
anahitaji kilichobaki kimoja ili awe juu Zaidi.
Kufikia
saa saba siku iliyofuata watu walimiminika kama kwa wingi na haraka sana kama
risasi zinazopigwa mfululizo, Mfalme alisimama mbele yao haya hakusubili
akalibishe na mlinzi wake bali aliwataka wananchi wa Hira kwa kusema samahani
wananchi leo kama kawaida yetu siyo siku maalumu kwa kukutana ilia nimewahitaji
huku nikitambua fika kuwa hapa kijijini tunavyovipawa vingi kwani mfalme
ninashida inayotakiwa itatuliwe na mmoja wenu hapa.
Mimi nimekuwa mtawala
wa kijiji hiki yapata miaka sabini sasa hivyo nimelidhika na kuwa mfalme japo
nitabaki kuwa mfalme lakini na hitaji mganga mmoja ambaye atanitengenezea pete
ambayo nikienda harusini baada ya muda nikiitazama nifurahi huliko yeyote pale
hata bwana harusi pia nikienda msibani nikiitazama nihuzunike kuliko wote hata
kumzidi yule baba mgane aliyeondokewa na mke wake kipenzi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment