UTUNZAJI WA MAZINGIRA
Wema Sepetu, Mbunge wa CHADEMA Devota Minja wapanda miti kuadhimisha siku ya wanawake Duniani
Wema amesema kupanda miti ni jambo ambalo linaleta tija kwa jamii yetu na hasa kupunguza kero ile kubwa ya maji inayotupa tabu wanawake.
“Leo ni siku ya wanawake Duniani, na kama mwanamke nikaonelea nijiunge na wanawake wenzangu wa Mkoa wa Morogoro siku ya leo katika upandaji wa miti ambao utakuja kuwa tija kwetu na kupunguza kero kubwa inayotukabili ya Maji,” aliandika Wema Instagram.
Aliongeza, “Wote tunajua kuwa mwanamke ndo anaekerwa zaidi katika upatikanaji wa maji… Labda haitotusaidia leo wala kesho, lakini itakuja kusaidia vizazi vyetu hapo baadae…. Morogoro ni eneo linalosadikika kuwa Chanzo cha Maji hata yale tunayotumia Mkoani kwetu (Daressalaam)… Ninajiskia faraja kuwa kutakuwa na helping hand yangu somewhere when it comes to Water supply in my society… Mazingira yetu hayana Itikadi wala Vyama, Yanagusa kila mtu… I feel honored to be part of this activity… Tumetoka Kata ya Kilakala and now tunaelekea kwenye Chanzo kingine kinachoitwa Mambogo…. For more pictures download my app only on Playstore…. #WemaApp #CallMeKamanda,”
The post Wema Sepetu, Mbunge wa CHADEMA Devota Minja wapanda miti kuadhimisha siku ya wanawake Duniani appeared first on Zanzibar24.
Zanzibar 24
No comments:
Post a Comment