CURRENCY CONVERTER

FreeCurrencyRates.com

New Ads

makala mbalimbali

BREAKING NEWS: Mzee Kingunge Ngombale–Mwiru Afariki Dunia ALFAJIRI YA LEO





Kingunge Ngombale Mwiru ni Mkongwe wa Tanzania na jina lake ni kubwa. Ni mstaafu ambaye katika maisha yake toka ujana wake amelitumikia Taifa mpaka hata ngazi za juu kabisa kama vile kuwa Mkuu wa Mkoa, Mbunge na hata Waziri.

Ni mmojawapo wa vijana wa TANU enzi zao hizo, walioshiriki harakati za kuutafuta uhuru mpaka ukapatikana. Yeye kingunge ndiye aliyekabidhiwa jukumu la kuzigawa kadi mia za kwanza kabisa za wana TANU baada ya TANU kuanzishwa ambapo, Bwana Sykes ndiye aliyezichapisha kwa pesa za kutoka mfukoni mwake.

Kingunge alifanya harakati akiwa karibu na Mwalimu Nyerere, na waliendelea kuwa karibu hata baada ya uhuru kwa majukumu ya kujenga Taifa changa. Kingunge alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa na nafasi nyeti katika TANU na CCM mpaka pale alipoamua kuondoka CCM wakati wa uchaguzi wa mwaka 2015 na kwenda upande wa upinzani.

No comments:

Post a Comment

Bottom Ad [Post Page]